IMEZIDI kuwa tamu balaa promosheni namba moja Bongo ya Chomoka na Gari inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publisher ambapo washindi watatu kesho wanakabidhiwa zawadi zao.

Ofisa Masoko wa Global Publisher, Anthony Adam amesema kuwa baada ya kucheza droo ya kwanza kwa mafanikio Machi 25 bado promosheni inaendelea na wasomaji wanapaswa kuendelea kutuma kuponi zaidi.

“Tulipata washindi watatu kutoka mikoa mitatu tofauti zawadi zao zimeshaandaliwa na kesho watakabidhiwa zawadi zao.

“Kwa wale wa mikoani ambao ni wawili, Swaleh Mohamed wa Tanga na Yesse Daniel ambaye ni mkazi wa Moshi hawa watakwenda kwa mawakala wa mjini kuchukua zawadi zao tayari zimefika na yule wa Dar Neema Chuma atachukua zawadi zake Dar,” amesema Adam.

Kushiriki promosheni hii ambayo inaendelea ni rahisi, nunua gazeti la Championi kwa 800 ama SpotiXtra kwa jero kisha ukurasa wa pili kuna kuponi utajaza na kumpa wakala aliye karibu nawe.  

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.