ALIYEWAHI kuwa kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere amesema kuwa aliamua kuondoka kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na wachezaji mastaa kutimka kila siku.

Wilshere amesema kuwa kila siku wachezaji mastaa wa Arsenal walikuwa wanaondoka na aliona kuwa kwenye timu hiyo hakuna mwanga.

Kiungo huyo ambaye aliwika zaidi msimu wa 2010-11, amesema alipoona mastaa kama Cesc Fabregas, Samir Nasri na Robin van Persie wanaondoka aliona kuwa kwenye timu hiyo kuna tatizo.

“Wachezaji wengine walikuwa wanauliza kwenye vyumba mbona wachezaji mastaa wanaondoka? Lakini hakuna aliyekuwa anatoa jibu sahihi.

“Niliona kuwa nami muda wa kuondoka umefika kwa kuwa niliona kila staa anaondoka na mwanga wa kuchukua makombe haukuwepo,” alisema Wilshere ambaye kwa sasa anaichezea West Ham.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.