PASCAL Wawa, beki kisiki wa Simba amesema kuwa anafurahia maisha yake ndani ya timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Kariakoo.

Wawa ni miongoni mwa mabeki ambao wamekuwa na uhakika na namba ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba kilicho chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa.

"Ninapenda maisha ndani ya Simba tunaishi kwa kushirikiana na kufanya kazi tukiwa ni timu ninaona kwamba bado ni sehemu salama kwangu.

"Soka la ushindani nimecheza kwa muda mrefu na timu nyingi hivyo kwa sasa bado nipo Simba na maisha yanaendelea," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.