WILLIAN Borges da Silva, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Chelsea iliyo chini ya Frank Lampard inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na Klabu ya Liverpool.
Nyota huyo mwenye miaka 31 hajaongeza mkataba mpya ndani ya Chelsea ambapo kumekuwa na mvutano kati yake na mabosi wake ambao wanataka kumpa dili la mwaka mmoja huku yeye akihitaji kupewa kandarasi ya miaka miwili.
Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp tayari imeanza hesabu za kuinasa saini yake ili kandarasi yake itakapomeguka ndani ya Chelsea aibukie Anfield
Post a Comment