FEISAL Salum, kiungo wa Yanga amesema kuwa anaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwa kufanya mazoezi binafsi.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na Serikali kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona yanayoitikisa dunia.
Fei amesema :"Kwangu mimi ni muhimu kuwa salama na kujilinda pia lakini ninachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na kuwalinda wenzangu.
"Ningependa kila mmoja kuendelea kuchukua tahadhari ili mambo yatakavyokuwa sawa tuwe pamoja kwani kwa sasa ninafanya mazoezi ili kulinda kipaji changu,".
Post a Comment