STAA wa Real Madrid, Gareth Bale amefunguka kuwa anatamani sana kurejea uwanjani, lakini suala la usalama wa afya ni muhimu kwanza.
  Hii ni kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa umeikumba dunia na kusababisha raia kukaa ndani ilikulinda usalama wao.
 Kwa sasa La Liga imesimama kutokana na hali hiyo  toka Machi na bado haijafahamika kuwa itarejea lini rasmi kutokana na  janga hilo.
 “Tumefungiwa ndani huwezi kutoka hata kutembea tu kwa ajili ya mazoezi na hata kufanya mazoezi imekuwa ni ngumu kutokana na hali ya sasa.
“Natamani kuona tunarudi tena uwanjani na sio mimi tu ni wengi wanatamani hivyo, lakini muhimu kuangalia afya zetu kwa sasa sababu Corona ni janga kubwa  nina tumaini kuwa wote tupo vizuri.
“Kitu kigumu kwa sasa unasikia kila mmoja anataka kuona msimu unamalizika, ila ukitafakari kwa umakini unaona kuwa afya za watu ni muhimu kuliko kingine.
“Tumemisi soka kulicheza na hata kuliangalia lakini ndiyo hivyo hakuna kitu kama hicho kwa sasa, ila naamini ipo siku kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Bale.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.