UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado una mkataba na nyota wao Mghana, Yakub Mohamed hivyo kama kuna klabu inamhitaji lazima utaratibu ufuatwe.
Habari zinaeleza kuwa mabosi wa Msimbazi, Simba wanaiwinda saini ya nyota huyo ambaye ni beki wa kati.
Abdulkarim Amin, Mtendaji Mkuu wa Azam FC amesema kuwa:"Yakub ni mali ya Azam FC kandarasi yake bado ni ya muda wa miaka miwili kwa kuwa aliongeza mkataba wake hivi karibuni.
"Ikiwa kuna timu inahitaji saini yake hakuna shinda ni suala la kukaa mezani kwani utaratibu upo wazi na hatujawahi kumzuia mchezaji anayetaka kuondoka ndani ya Azam FC,"
Post a Comment