PASCAL Wawa raia wa Ivory Coast amesema kuwa kwa sasa amekuwa akitumia muda mwingi katika upishi kwa kujipikia vyakula anavyopenda kila baada ya kumaliza mazoezi kutokana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona.
Wawa ametoa kauli hiyo kutokana na kitendo chake cha kuonyesha video zake katika mitandao ya kijamii akiwa anapika vyakula vyenye asili ya kwao kila baada ya kutoka mazoezini.
Wawa amesema kuwa kwa sasa anatumia muda wake kufanya mazoezi binafsi na kupika.
“Kiukweli napenda kupika, napenda sana ndiyo maana umeona hizo video nikiwa naandaa chakula changu ninachopenda na inakuwa inanipa urahisi wa kujua nini nataka kula.
“Unajua suala la kupika kwangu ni jambo la kawaida kwa sababu nimekuwa nikipenda kufanya hivyo na kwa sasa nimekuwa nikifanya mazoezi halafu nageukia mapishi hakuna kitu kingine cha kufanya kwa sababu ya Corona ambayo imezuia kila kitu,” amesema Wawa ambaye ni beki mwenye pasi moja ya bao kati ya mabao 63
Post a Comment