SERIKALI ya Uingereza inaelezwa kuwa ipo kwenye mpango wa kutazama upya namna bora ya kurejesha Ligi Kuu England ili kurudisha furaha kwa mashabiki wa mpira duniani ambao wamewekeza mawazo mengi kwa sasa kwenye maambukizi ya Virusi vya Corona.
Ligi Kuu England ilisimamishwa Machi 13 na mpaka sasa hakuna anayejua hatma yake itakuaje huku mpango wa kwanza ukipangwa kumaliza mechi zilizobaki za msimu huu kwa timu kucheza bila kuwa na mashabiki.
Serikali imesema kuwa kuna mambo mengi ya kufanya ambayo yamesimama kutokana na maambukizi ya Corona hivyo kuna namna ambayo wanapaswa wafanye ili kurejesha mambo kwenye hali yake ya zamani.
Juni 8 inatazamiwa mechi nyingi kuanza kuchezwa ambapo kwa sasa mpango huo unashidikana kwa kuwa bado kuna maambukizi mapya yanaendelea ya Virusi vya Corona.
Mpango utatoa pia wiki tatu za maandalizi kwa timu kabla ya ligi kuanza ili kumaliza msimu wa 2019/20 ambapo wachezaji watapewa nafasi ya kufanya mazoezi kwa pamoja tofauti na ilivyo sasa ambapo wachezaji wapo majumbani kwao.
Wakati Ligi Kuu England inasimamishwa vinara walikuwa ni Liverpool ambao walijikusanyia pointi 82 baada ya kucheza mechi 29.
Post a Comment