BORUSSIA Dortmund imeripotiwa kuwa imeanza mazungumzo na mchezaji wao Jadon Sancho ili aongeze mkataba wake kuendelea kubaki Klabuni hapo.
Nyota huyo mwenye miaka 20 amekuwa akipigiwa hesabu na timu nyingi ambazo zinashiriki Ligi Kuu England.
Manchester United na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuiwinda saini ya nyota huyo.
Mkataba wake wa sasa unameguka mwaka 2022 hivyo mabosi wa Dortmund wanataka wamuongeze mkataba wa mwaka mmoja ili adumu klabuni hapo mpaka 2023 huku wakiongeza na dau la malipo kwake
Post a Comment