SELEMAN Matola ndani ya Simba msimu huu ameongoza timu hiyo kwenye mechi 18 akiwa ni Kocha Msaidizi baada ya kujiunga na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea Polisi Tanzania.
Ameshuhudia JKT Tanzania na Yanga zikisepa na pointi sita mazima baada ya kupoteza mechi hizo kwa kuambulia kichapo cha maana.
JKT Tanzania ilimtungua Beno Kakolanya bao 1-0 Uwanja wa Uhuru na Yanga ilimtungua Aishi Manula bao 1-0 Uwanja wa Taifa.
Matola akiwa benchi pia ameshududia wakigawana pointi moja na Yanga Uwanja wa Taifa kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Tabasamu lake lilionekana kwenye mechi 15 ambapo walisepa na pointi 45 mazima baada ya kushinda kibabe ndani ya ligi.
Akiwa kwenye benchi ni Yanga wamempa tabu kubwa msimu huu tofauti na msimu uliopita alipokuwa Lipuli ambapo aliwabana mbavu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho msimu huu hajapata bahati ya kusepa na pointi tatu kwenye timu zote mbili.
Alipokuwa Polisi Tanzania alikubali sare ya kufungana mabao 3-3 na kugawana pointi moja na alipoibukia Simba ameambulia pointi moja na moja amechapwa.
Hatimaye leo anaongeza miaka kadhaa, heri ya kuzaliwa Seleman Matola
Post a Comment