ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa iwapo wachezaji watashindwa kufanya mazoezi binafsi wakati huu wa mapumziko ya lazima kuna hatari ya viwango vyao kuporomoka.
Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na wachezaji wapo nyumbani wakifanya mazoezi binafsi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kufanya mazoezi aliyopewa iwapo hawatazingatia ni rahisi kwao viwango vyao kuporomoka.
"Muhimu kwa wachezaji kufanya mazoezi binafsi, iwapo watashindwa kufanya mazoezi kwa sasa itakuwa ni rahisi kwao viwango vyao kushuka pale ligi itakaporejea.
"Ninaamini wachezaji wamepewa program maalumu kwa ajili ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona, ila wakati huu ni muhimu kulinda vipaji vyao," amesema.
Post a Comment