SELEMAN Matola, Kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa ni ngumu kwa sasa kufuatilia maendeleo ya wachezaji iwapo wanafanya mazoezi au la wakiwa nyumbani.

Baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na Serikali Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona wachezaji wapo nyumbani baada ya kambi kuvunjwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa hakuna anayeweza kuwafuatilia wachezaji wa Bongo kutokana na mazingira yaliyopo.

"Ni ngumu kuwafuatilia wachezaji wakiwa nyumbani kutokana na mazingira yaliyopo hasa kwetu sisi kibongobongo tunaelewa namna mambo yalivyo.

"Lakini haina maana kwamba kwa kuwa hakuna namna ya kuwafuatilia basi wasifanye mazoezi haitakuwa sawa, mazoezi wafanye na tahadhari wachukue" amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.