MIAMBA ya soka ndani ya Ligi Kuu England ikiwa ni pamoja na Liverpool, Manchester United na Arsenal imegongana kwenye kuwania saini ya nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Monaco, Wissam Ben Yedder.
Ben Yedder ambaye alijiunga na AS Monaco akitokea Klabu ya Sevilla amekuwa ni nyota ndani ya Ligue 1 msimu huu ambapo ametupia mabao 18 akiwa amecheza mechi 26.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 amezivutia klabu nyingi kubwa ambazo zinahitaji kuipata saini yake kwa ajili ya kumtumia msimu ujao wa 2020/21.
Mbali na timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England inaelezwa kuwa timu zinazoshiriki La Liga pia zinahaha kuipata saini ya nyota huyo huku Real Madrid ikitajwa kuwa mstari wa mbele huku kwa upande wa zile za Ligi Kuu England, Manchester United, Liverpool, Tottenham na Arsenal zikitajwa kuiwinda saini ya nyota huyo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.