BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ataendelea kulinda kipaji chake kwa kufanya mazoezi ili kuwa bora zaidi.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Morrison anafanya mazoezi binafsi akiwa nyumbani na muda mwingine amekuwa akitumia kufanya mazoezi hayo katika Uwanja wa Chuo cha Sheria.

Morrison amesema:"Ni jukumu langu kulinda kipaji changu na hali ilivyo kwa sasa ni muhimu pia kuchukua tahadhari, kikubwa ninachokifanya ni kulinda kipaji changu na kuchukua pia tahadhari.

"Imani yangu pale ligi itakaporejea nitakuwa kwenye ubora wangu na nitaendelea pale ambapo niliishia," amesema.

Kwenye ligi Morrison ambaye ni ingizo jipya alisajiliwa kwenye dirisha dogo la mwezi Januari amepachika mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.