WAZIRI Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, ametangaza kuwa, michezo yote ndani ya nchi hiyo imesimamishwa hadi Septemba Mosi, mwaka huu.

Kutokana na hilo, inamaanisha kwamba Ligi Kuu ya Uholanzi maarufu Eredivisie pamoja na ligi zingine nazo zimepigwa ‘teke’ hadi muda huo, hivyo hakutakuwa na michezo kwa takribani miezi mitano ijayo.

Viwanja vyote vya soka vitatakiwa kufunguliwa Septemba Mosi, hivyo msimu huu wa 2019/20 nao utaendelea muda huo. Kwa sasa hapana. Hii yote inatokana na uwepo wa janga la corona.

"Ni ngumu, lakini tunapaswa kufanya hivyo," alisema Rutte.

Hadi ligi hiyo inasimamishwa, timu nyingi zilikuwa zimecheza mechi 26 na kubakiwa na nane tu kumaliza msimu huu wa 2019/20 huku vinara wakiwa Ajax waliocheza mechi 25 na kukusanya pointi 54 sawa na AZ Alkmaar wanaoshika nafasi ya pili.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.