ABDI Banda, beki anayekipiga soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Highlands Park FC amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kufanya mazoezi wakiwa ndani huku wakifuatiliwa na makocha wao kwa ukaribu.
Ligi Kuu nchini Afrika Kusini imesimamishwa kwa muda kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wanafanya mazoezi wakiwa nyumbani.
Banda amesema:-"Tunaendelea na mazoezi kama kawaida lakini sio kama ilivyokua mwanzo ambapo tulikuwa tunasimamiwa na makocha, kwa sasa kila mmoja anafanya mazoezi akiwa nyumbani lakini taarifa zake anatuma kwa makocha kupitia mtandao.
"Kikubwa ambacho tunakifanya ni kila mmoja kuwa na nidhamu ya kile ambacho ameambiwa afanye pale ambapo anashindwa anaomba maelekezo kutoka kwa kocha wake anayemsimamia." amesema
Post a Comment