AMIS Tambwe, mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba amesema kuwa Yanga inahitaji kufanya usajili makini ambao utawapa matokeo chanya msimu ujao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Tambwe ambaye msimu uliopiota akiwa ndani ya Yanga alifunga mabao 12 amesema kuwa anaamini viongozi wanatambua aina ya wachezaji ambao wanawahitaji.

"Nimekuwa Yanga na ninatambua kwamba kuna viongozi ambao wanajua wajibu wao hivyo ni muhimu kwao kufanya usajili makini kwa ajili ya msimu ujao.

"Kwa sasa ni jambo la kuomba Mungu hali iwe shwari na ligi irejee kwani maambukizi ya Virusi vya Corona yamesimamisha mambo mengi kwenye dunia," amesema.

Mabao nane Tambwe alifunga kwenye ligi huku manne akifunga kwenye Kombe la Shirikisho

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.