BAADA ya juzi Alhamisi, Azam FC kumuongezea mkataba mshambuliaji wa klabu hiyo, Obrey Chirwa, inaelezwa kuwa timu hiyo haina mpango wa kumuongezea mkataba nyota wake, Donald Ngoma.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Azam FC zinadai kuwa, Ngoma amekuwa hana mwendelezo mzuri ndani ya klabu hiyo kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara hali inayofanya ashindwe kuonyesha kiwango bora na kutoa mchango wake kwenye timu kwa asilimia 100.
Mtu wa karibu kutoka ndani ya Azam FC, aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Ngoma alitakiwa arejee Dar kuja kuongeza mkataba sambamba na mwenzake Chirwa, lakini viongozi wameona bora amalize mkataba wake aondoke na wao watafute mshambuliaji mwingine, hiyo inatokana na uwezo wake kushindwa kuongezeka kutokana na majeraha ya mara kwa mara
Post a Comment