LICHA ya kukaa kwa siku chache na wachezaji wake kambini Morogoro, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, amekoshwa na kasi ya wachezaji wake katika kambi hiyo.

Zahera alitua nchini wiki iliyopita na kwenda moja kwa moja Morogoro kwa ajili ya kuangalia kambi hiyo ambapo wakati anafika Yanga walikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market ya Morogoro.

Katika mchezo huo, Yanga walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Issa Bigirimana lakini alikuwepo kwenye mchezo mwingine dhidi ya Friends Rangers ambao Yanga walishinda kwa mabao 2-0. Katika kambi hiyo winga mpya, Patrick Sibomana ndiye aliyeongoza kwa kufunga mabao mengi akifunga matano akifuatiwa na Mganda Juma Balinya aliyefunga manne.


Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh ameliambia Championi Ijumaa, kuwa Zahera amekoshwa na wachezaji wapya wa Yanga wanaoongoza na mastraika hao wawili.

“Kocha Zahera licha ya kwamba hakuwepo hapa Morogoro lakini alikuwa anatuma programu kwa Mwandila, kwa hiyo wakati alipofika alikuta kila kitu kiko sawa na hakukuwa na
mabadiliko yoyote yale.

“Yeye amekuja tu kuendeleza kile ambacho alikuwa anamtumia Mwandila, kwa hiyo hakuwa na kazi kubwa wala mabadiliko yoyote aliyoyafanya tangu alipofika. “Alichokuwa anakifanya ni kuangalia wachezaji tu, kwani waliposajiliwa hakuwepo na ameona wachezaji wote wako vizuri na amekoshwa na namna walivyo,” alisema Hafidh.

MARCO MZUMBE NA SAID ALLY, Dar

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.