PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezo wake dhidi ya UD Songo utakuwa mgumu na amejipanga kufanya vizuri hivyo mashabki wajitokeze kwa wingi.

Kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Simba ililazimish sare tasa ya 0-0 na UD Songo nchni Msumbiji hivyo wana kazi ya kutafuta ushindi Agosti 25 uwanja wa Taifa.

"Kwa sasa tunaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wetu wa marudiano kwani baada ya kumalizana na Azam FC hesabu zetu ni kwenye mchezo wetu wa marudio.

"Bado sijajua kama nitamtumia mchezaji wangu John Bocco nadhani nikipata ripoti nitajua hatma yake," amesema.

Bocco alipata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC uwanja wa Taifa alishindwa kumaliza kipindi cha kwanza nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama ambaye alifunga bao la 3 kwenye ushindi wa mabao 4-2.
Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.