10. Toby Alderweireld (Tottenham)

Alderweireld alipitia kipindi kigumu Spurs wakati mkataba wake ulipofikia ukingoni msimu 2017/2018. Hata hivyo, alithibitisha ubora wake katika fainali za Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ubelgiji ambapo timu yake ilishika nafasi ya tatu.

Baada ya kutoka katika fainali hizo aliivutia Manchester United, lakini kocha Mauricio Pochettino alimuwekea nguvu. Wachezaji wenzake Spurs na Ubelgiji wanamtaja Alderweireld ni beki hodari mwenye uwezo wa kupambana na washambuliaji watukutu.

9. Jan Vertonghen (Tottenham)

Baada ya kudumu Spurs kwa misimu saba, Vertonghen anatajwa ni mmoja wa mabeki hodari wa kati duniani. Vertonghen anatengeneza pacha na Alderweireld katika safu ya mabeki wa kati. Beki huyo anatajwa ni hodari wa kucheza ‘mtu na mtu’ katika safu ya ushambuliaji.

8. Giorgio Chiellini (Juventus)

Ingawa nguli huyo atatimiza miaka 35 mwezi ujao, lakini bado ni beki shupavu katika kikosi cha Juventus.

Chiellini ni hodari wa mipira kupiga laza kwa washambuliaji wenye kasi ya kuambaa na mpira pembeni mwa uwanja.

Nguli huyo ni beki kiongozi uwanjani na amekuwa katika michuano ya Ulaya tangu mwaka 1996.

7. Diego Godin (Inter Milan)

Godin si beki wa kati anayeweza kukonga nyoyo za makocha kama Pep Guardiola au Maurizio Sarri, kutokana aina ya uchezaji wake.

Lakini anafiti kwa kocha kama Diego Simeone wa Atletico Madrid ambaye ni muumini wa mabeki wanaotumia zaidi nguvu.

Beki huyo wa zamani wa Villarreal mwenye miaka 33, alitua Inter Milan msimu uliopita.

6. Gerard Pique (Barcelona)

Pique ana kila sababu ya kujivuniaBarcelona akiwa ni mmoja wa mabeki hodari wa kati.

Mhispania huyo ametwaa kila aina ya makombe Barcelona. Licha ya kuwa na miaka 32, nguli huyo bado ni kiongozi katika safu ya ulinzi.

Pique anaunda ngome imara na beki Clement Lenglet, lakini alianza kupikwa wakati akicheza na aliyekuwa nahodha wa Barcelona, Carles Puyol.

5. Aymeric Laporte (Manchester City)

Laporte ni aina ya beki ambaye anafaa kucheza chini ya Guardiola kwa aina ya uchezaji wake wa kiingereza. Laporte, aliyejiunga na Athletic Januari 2018.

4. Sergio Ramos (Real Madrid)

Licha ya ukongwe wake nahodha wa Real Madrid anabaki kuwa beki bora duniani akiipa kila aina ya mataji klabu hiyo ya Santiago Bernabeu.

Hata hivyo, Ramos amekuwa katika mzozo wa muda mrefu na waamuzi kutokana na kupewa kadi nyekundu mara kwa mara. Pamoja na kasoro hiyo beki huyo amefunga mabao 59.

3. Kalidou Koulibaly (Napoli)

Napoli ilimpoteza Jorginho kwa Chelsea msimu uliopita majira ya kiangazi. Lakini yupo beki anaitwa Koulibaly ambaye ameingia katika orodha ya mabeki bora duniani.

Beki huyo wa kimataifa wa Senegal ana uwezo kuziwahi pasi, kuruka juu na hodari wa kutibua mipango ya washambuliaji.

2. Raphael Varane (Real Madrid)

Varane ni beki hodari ambaye mchango wake Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa utakumbukwa.

Beki huyo wa kati ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne na Ligi Kuu Hispania mara mbili.

Varane ni beki wa kati asilia aliyejenga ngome imara na nahodha wake Sergio Ramos. Beki huyo amekuwa akiziba makosa ya mabeki katika safu ya ulinzi.

1. Virgil van Dijk (Liverpool)

Hakuna ubishi Virgil van Dijk ndiye beki bora duniani kwasasa akiwa na kila aina ya mafanikio Liverpool. Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi, ameipa Liverpool ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Awali, Jurgen Klopp alipata upinzani mkali alipoa Pauni75 milioni kupata saini yake akitokea Southampton. Mholanzi huyo anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia akiwania kufikia rekodi ya nyota wa zamani wa Juventus, Fabio Cannavaro aliyotwaa mwaka 2006.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.