Shangwe na vifijo zinaendelea mtaa wa Msimbazi pembeni kidogo kwenye kituo cha Mwendokasi , kwenye lile jengo lililo na Mama Ntilie kwa chini kabla ya kupanda ngazi. Shangwe lao linakuja baada ya kunyanyua ngao ya Hisani kwa kuwachapa Wanalamba lamba 4-2.
Licha ya ushindi huo, sio wote wanafuraha mtaani hapo karibu na kituo cha Polisi cha Msimbazi.
Na hili limethibitishwa baada ya siku za hivi karibuni kupitia Msemaji wa timu hiyo pale alipoyabwaga ya moyoni baada ya kutemwa kwenye nafsi yake na kuchukuliwa na bwana mdogo Gift
Aliandika
Waandishi wanauliza!
Instagram swali ni hilo hilo!
Magroup ya WhatsApp ndio usiseme!!
Fanyeni subira,Jumatatu ntaongea na Press Insha’Allah ,baada ya kesho kushauriana na familia yangu
Hebu tuachane na hilo kwanza!
Siku ya jana baada ya Wekundu hao wa msimbazi kunyakua Ngao ya Hisani, camera za Azam Tv zilimumlika msemaji wa Simba akiwa hana furaha na hata alipojaribu kupretend alionekana kabisa hana mood kama alivyozoeleka na baadhi ya wadau nilikuwa naangalia nao mpira akiwemo mwandishi nguli Peter Mbaga nae alinidokeza jambo hili
Mcheki mcheki Manara hana mood kabisa na hii inaweza tokana ana ile ishu yake aliongezea Peter Mbaga
Sawa licha ya hilo wachezaji mbalimbali wa klabu hiyo walionekana kushangilia kwa namna mbalimbali akiwemo pia msemaji huyo ambae alioonekana kushangilia kwa namna ya kipekee kwa kujifanya anazichapa na mchezaji wa Team hiyo, Jonas Mkude.
Hii ilitafsriwa na mashabiki mbalimbali mtandao wakidai jamaa anammalizia hasira mchezaji huyo ha ha ha!
Cheki mwenyewe;
tentenchelsea Hii ni Tanzania pekee timu ina msemaji na anaingia uwanjani kupokea medali hahahaha
brytonkelvin Angempa moja tu ya nguvu yy wangegawan majengo ya serekali mmoja mochwar mwengine jela
Post a Comment