LONDON, England
SEPTEMBA 12, mwaka huu klabu za Ligi Kuu England zitakutana kujadili kuhusu lini dirisha la usajili lifungwe.
Timu hizo zilimaliza biashara zao za usajili kabla ya saa 1 usiku, Agosti 8, siku moja kabla ya Ligi Kuu England kuanza lakini sehemu zingine dirisha la usajili litafungwa Septemba 2.
Taarifa zinadai kwa asilimia kubwa klabu hizo za England zipo tayari kuongeza muda wa usajili kama ilivyokuwa zamani na kuwa sawa kama ligi zingine Ulaya.
Kama makubaliano yakishindwa kufikiwa, kutakuwa na kikao kingine ambacho kitafanyika November ambacho kitakuwa cha mwisho kutoa mustakabali wa dirisha la usajili.
Mwaka 2017, timu sita tu zilichagua kuendelea na mfumo wa zamani, ambazo ni Manchester United, Manchester City, Burnley, Swansea, Watford na Crystal Palace. Huku 14 zilichagua mabadiliko ya usajili.
Inahitaji makubaliano ya timu 11 na zaidi ili sheria ya usajili ibadilishwe, mpaka sasa kumekuwa na malalamiko mengi ya wachezaji kutoka England kuhitajika na timu kutoka nje ya ligi hiyo ambayo usajili unakuwa haujafungwa.
Post a Comment