Kagere alifanya mazoezi ya kunyosha viungo kwa muda mfupi kisha akaenda kukaa huku wenzake wakiendelea na kuchezea mipira.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amekaa pembeni akishuhudia wenzake wakifanya mazoezi kwenye viwanja vya Gmykhana jioni hii.

Simba inajiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo, itakayopigwa Jumapili ya wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kagere alifanya mazoezi ya kunyosha viungo kwa muda mfupi kisha akaenda kukaa huku wenzake wakiendelea na kuchezea mipira.

Kagere alionekana kuwa na umakini wa kufuatilia kile kilichokuwa kinafanywa na wenzake, akionekana ana mzuka na kinachoendelea.

Achana na kutofanya kwake mazoezi Kagere akifunga bao ana staili ya kuonyesha dole gumba la mkono wake wa kulia chini, amendeleza vituko hivyo kwa mashabiki ambao walikuwa wakimtazama.

Tags: ,

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.