- Nyota wa Brazil, Neymar anaendelea kuwavutia mabingwa wa Uhispania Real Madrid

- Wakuu wa Los Blancos wanasemekana kuwatuma mawakilishi wao jijini Paris kufanya mazungumzo

- Mzaliwa huyo wa Brazil pia amehusishwa na kurejea kwa miamba wa Uhispania Barcelona

Miamba wa Uhispania, Real Madrid, wanaripotiwa kuwatuma mawakilishi wao jijini Paris kufanya mazungumzo na klabu ya Paris Saint-Germain, kuhusu usajili wa Neymar.

Neymar anasemekana kukataa kuendelea kuichezea PSG, msimu huu na amekuwa akihusishwa na kurejea Barcelona.

Nyota wa timu ya Brazil na PSG Neymar wakati wa mazoezi nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa Sun (UK), Real Madrid wako tayari kuafikiana na ofa ya vigogo hao wa Ufaransa ili kumnasa Neymar kuelekea Madrid.

Hata hivyo, huenda PSG wakafaulu kumshawishi Neymar kusalia Aris, huku ripoti zikiarifu kuwa majenti wa staa huyo, babake na PSG wameboresha uhusiano kwa siku kadhaa sasa.

Guillem Balague

@GuillemBalague

Barcelona AND Real Madrid have been asked to put a final offer before midday today. Juventus also in the equation.

The latest twist: in the last few days the relationship between #Neymar, his father/representative and #PSG has improved dramatically (in a VERY positive way)

386

11:28 AM - Aug 23, 2019

Twitter Ads info and privacy


169 people are talking about this

Ripoti hiyo pia inadokezea kuwa PSG wako tayari kumruhusu Neymar kuondoka kwa mkopo msimu huu wa ada ya pauni 200 milioni na kisha baadaye kusajiliwa kwa muda.

Barcelona na Real Madrid wamegharamika sana msimu huu, lakini Los Blancos wametumia kiasi cha pauni 100m kununua talanta.

Awali, TUKO.co.ke iliripoti kuwa nguli wa timu ya taifa ya Brazilian Rivaldo alimuhimiza Neymar kuondoka PSG msimu huu na pia kubadilisha mtindo wake wa maisha.

Hatma ya Neymar katika klabu ya PSG inayumba huku duru zkiarifu kuwa amekubali ofa ya kurejea Barcelona.

Staa huyo aliyeondoka Barcelona miaka miwili iliyokwisha, anaripotiwa alikuwa amechoshwa kwa kucheza kama mchezajiwa akiba katika nafasi ya Lionel Messi ugani Nou Camp.

Source: Tuko

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.