Na Shabani Rapwi
Klabu ya Real Valladolid imekamilisha usajili wa mlinda mlango wa kimataifa wa Ukraine, Andriy Lunin kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka klabu ya Real Madrid.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Real Madrid msimu wa mwaka 2018 kutoka FC Zony Luhask ya Ukraine kwa mkataba wa miaka sita.
Lunin msimu uliopita alishinda tuzo ya mlinda mlango bora (Golden Glove) katika michuano ya Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 20 yaliofanyika nchini Polando na timu ya Taifa ya Ukraine kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa kuifunga Korea Kusini mabao 3-1 katika mchezo wa fainali.
Post a Comment