Kocha wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ametamba juu ya mavazi yake ambayo huwa anatupia kila mara uwanjani.
Akizungumza jana amesema kuwa yeye huwa anapenda kuvaa kaptula kila mara na hasa zile ambazo zinapatika kila mahali aendapo.
"Si mnajua mimi kila mara navaa Polo hiyo ndio mimi navaa kwenye mechi zote za ligi. Napenda tu kuvaa vitu vinavyotengenezwa na kampuni ya Polo sio kampuni nyingine ambazo zipo kilamahali hata Kariakoo unapata," amesema.
Alipoulizwa kuhusu kocha wa Simba SC ambaye mara nyingi huvaa Shati Jeupe akiamini ni rangi ya bahati kwake, alijibu; "Ni maamuzi ya mtu binafsi, mimi naweza kuamua kutembelea gari aina ya Mercedes lakini sio kila mtu atapenda kwa hiyo kama yeye anapenda kuvaa shati jeupe sawa lakini mimi ni mvaaji wa bidhaa za Polo."
Post a Comment