BAADA ya Simba kutolewa katika michuano ya kimataifa, kiungo wa timu hiyo, Said Ndemla amesema kuwa inahitajika juhudi kubwa kwa sasa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.
Mchezaji huyo awali alikuwa akitegemea kupata nafasi katika kikosi cha kwanza endapo wachezaji wengine watakuwa wameiwakilisha Simba katika michuano ya kimataifa, jambo ambalo kwa sasa halipo kutokana Simba kutolewa.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ndemla alisema kuwa Simba ina wachezaji wengi sana haswa katika eneo la kiungo, msimu uliopita alipata nafasi baada ya wachezaji wengine kupumzishwa kutokana na kucheza mechi za kimataifa, hivyo baada ya Simba kutolewa mapema itabidi ajitume zaidi ili apate nafasi ya kucheza.
“Simba kuna wachezaji wengi kwenye eneo la kiungo, msimu uliopita nilipata nafasi ya kuanza kwenye mechi ya ligi kutokana na wachezaji wengine kutoka kwenye mechi za kimataifa, msimu huu tumetoka mapema hivyo hakuna jinsi itabidi nipambane ili nimshawishi kocha anipe nafasi,” alisema Ndemla.
Post a Comment