MOHAMED Abdallah ‘Bares’ Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa wapo tayari kusepa na pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa kwanza utakaochezwa uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema wanaiheshimu Simba ila wamejipanga kufanya kweli mchezo wa leo wa ligi.
“Tunatambua ubora wa Simba hasa ukizingatia kwamba imetoka kushiriki michuano ya kimataifa si timu ya kubeza, nimemaliza programu maalumu kwa wachezaji na nimewaambia kazi ya kufanya.
“Tunataka kuanza ufunguzi kwa heshima ndio maana tunaifuata Simba kwa nidhamu na adabu ila kikubwa ni pointi tatu muhimu hakuna jambo jingine tunalofikiria, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Msimu uliopita JKT Tanzania iliacha pointi zote sita mikononi mwa Simba baada ya kufungwa mchezo wa kwanza ikiwa nyumbani mabao 2-0 na mchezo wa pili bao 1-0.
Post a Comment