SAKATA la beki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ limeibua mjadara mpya baada ya mchezaji huyo kushangazwa na uongozi wa klabu hiyo kumpunguzia fedha anazowadai.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema mchezaji huyo anadai 18 milioni ambazo walimuomba wampunguzie kwa kumlipa kumi ili nane.

Alisema baada ya mazungumzo hayo na mchezaji huyo alikataa na kutaka alipwe fedha yake yote kitu ambacho kwa wakati huo uongozi ulikuwa hauna na kuamua kumruhusu kuondoka wakiahidi kumuita tena.

“Dante na Juma Abdul ndio wachezaji ambao waligoma wakishinikiza kulipwa madeni yao tulifanya makubaliano kwa kuwaita wachezaji wote na kuwomba kuwapunguzia madai yao, Abdul alikubali kidogo tulichompa lakini Dante aligoma,” alisema na kuongeza kuwa:

“Baada ya mchezaji huyo kukataa tulimuacha jijini na Abdul tulisafiri naye kambini Arusha tulivyorudi tulimuita tena mchezaji huyo kwa ajili ya makubaliano hakuweza kutokea kwa madai kuwa yupo katika matatizo anamuuguza mama yake,” alisema.

Mwanaspoti lilimtafuta Dante ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema anashangazwa na tukio la kupunguziwa deni na kuweka wazi kuwa yeye anaidai klabu hiyo zaidi ya 45 milioni ambazo ni malimbikizo ya mishahara ikiwa na fedha ya usajili wa msimu huu wa mwaka 2019/20.

“Ni kitu cha kushangaza naambiwa nadai 18 milioni wakati nawadai fedha ya usajili sambamba na malimbikizo ya mishahara na kuhusiana na kuniita kwaajili ya kumalizana mara ya pili ni kweli niliwaambia nauguza lakini nilimtuma mwanasheria wangu ili aweze kulisimamia hilo,” alisema na kuongeza kuwa:

“Mwanasheria wangu kaenda zaidi ya mara tatu bila ya kuonana na makamu mwenyekiti na hivi leo (jana Alhamisi) tunavyozungumza yupo klabuni kwaajili ya mazungumzo na viongozi kwa ajili ya kukubalina ni namna gani watanilipa madai yangu,” alisema Dante.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.