Na Shabani Rapwi

MLINDA Mlango wa klabu ya Real Madrid, Keylor Navas anakaribia kutua PSG baada ya Madrid kukubali ombi lake la kutaka kwenda kucheza kikosi cha kwanza nje ya klabu hiyo.

Navas amechukua uwamuzi huo baada ya kocha Zinedeni Zidani kuweka wazi msimamo wake kwamba Thibaut Courtois ndio atakuwa mlinda mlango wake namba moja msimu huu 2019/2020.

Navas mwenye umri wa miaka 32 nafasi yake ya kuanza golini ilianza kupotea mara baada ya kuteuliwa Santiago Solari kuwa kocha mkuu wa Madrid na chaguo lake la kwanza lilikuwa kwa mlinda mlango Thibaut Courtois.

Navas alijiunga na Madrid mwaka 2014 kutoka klabu ya Levante na alianza kucheza rasmi kikosi cha kwanza msimu wa 2015/2016 na kutwaa mataji ya klabu bingwa barani ulaya mara tatu mfululizo akiwa mlinda mlango namba moja.

Nae kocha wa PSG, Thomas Tuchel amesema anataka mlinda mlango wa daraja la juu kama Navas ili kumsaidia katika harakati zake za kufanya vizuri katika klabu bingwa ulaya.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.