Emmanuel Okwi ametambulishwa rasmi Itthad Alexandria ya nchini Misri na kukabidiwa jezi namba 19 tofauti na namba 7 ambayo alikuwa akiitumia alipokuwa Simba.
Ruvu Shooting hawana hamu naye kwani misimu miwili ambao ni ule wa mwaka 2017/18 na 2018/19 amewapiga 'hat trick' mara mbili kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara.
Alifunga jumla ya mabao 15 msimu wa 2018/19 na alibeba tuzo ya mfungaji bora msimu wa 2017/18 baada ya kutupia jumla ya mabao 20.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Okwi ni miongoni mwa wachezaji bora ndani ya Simba kutoka nje.
"Okwi ni miongoni mwa wachezaji bora ambao wamepita ndani ya Simba wa kigeni, tutamkumbuka na tunamtakia kila la kheri,".
Post a Comment