Mchezaji wa Brazil Gabriel Jesus amefungiwa kucheza soka ya kimataifa kwa miezi miwili kutokana na tabia chafu aliyoionesha baada ya kutolewa nje katika mechi ya michuano ya kombe la Copa America mwezi uliopita.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City alifunga goli kwenye mechi waliyoshinda 3-1 dhidi ya Peru alijibizana na refa Roberto Tobar, kupiga teke chupa ya maji na baadaye kuisukuma mashine ya VAR wakati anaondoka kiwanjani.
Jesus, ambaye pia amerambwa faini ya dola za kimarekani 30,000, ana siku saba za kukata rufaa. Mshambuliaji huyo anatarajiwa kukosa mechi ya kirafiki dhidi ya Colombia na Peru zitakazopigwa mwezi Septemba.
Post a Comment