BAADA ya kuwa nje kutokana na majeraha na kurejea kwenye mazoezi straika wa Simba Ibrahim Ajibu, amefunguka kuwa ameanza mazoezi atawakosa UD Songo ila mechi zijazo atakuwa fiti kupambana na kuisaidia timu yake.
Ajibu ambaye amesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Yanga, alipata majeraha akiwa na timu ya Taifa na alishindwa kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa dhidi ya UD do Songo.
Simba itacheza mchezo wake wa marudiano wa kimataifa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Msimu uliopita nyota huyo akiwa Yanga aliweka rekodi yake ya kutoa asisti 17 na kufunga mabao sita, huku timu yake ikimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ajibu alisema ameanza mazoezi yake hivi karibuni lakini hayuko fiti kuweza kupambana kwenye mchezo ujao.
“ Kwa sasa ninaendelea vizuri na nimeanza mazoezi hivi karibuni lakini sipo fiti kwa mchezo ujao na Ud Songo hivyo najipanga kuwa fiti zaidi ili kuona naisaidia timu yangu kwenye michezo ijayo.
“ Kukaa nje hakuna anayependa ni ngumu lakini wakati mwingine inabidi kutokana na majeraha ni jambo ambalo halizuiliki hata kidogo,”alisema Ajibu.
Post a Comment