Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amekataa kuwazungumzia Zesco United hivi sasa na badala yake akili yake inafikira mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Zahera ameeleza hayo baada ya kikosi cha Yanga kuwasili jijini Dar es Salaam kikitokea Bostwana kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers.
Akizungumza mbele ya wanahabri, Zahera ameeleza kwa sasa mipango yao ni kuiwazia Ruvu na si Zesco United.
"Mimi naangalia mechi yetu ijayo na Ruvu, hawa Zesco siwezi kuwazungumzia kwa sasa.
"Tunapaswa kuingia kambini kwa ajili ya mechi hiyo kabla ya kukutana na Zesco maana ni muhimu zaidi," amesema Zahera.
Post a Comment