Mshambuliaji wa Manchester United amefikia uamuzi wa kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 2.




London, England. Muda mfupi baada ya Manchester United kutaka kumpeleka Alex Sanchez kwa AS Roma, mshambuliaji huyo anayetaka AC Milan au Juventus.


Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer alisema AS Roma ni klabu anayofaa kujiunga nayo endapo watakubaliana kumtoa kwa mkopo.


Sanchez ameonyesha hana nia ya kubaki Man United baada ya kudai anataka kuondoka kabla ya dirisha la usajili UIaya kufungwa Septemba 2.


Mchezaji huyo wa kimataifa ana matumaini ya kutua AC Milan, Napoli au Juventus.


Sanchez ana hali ngumu Man Unitedm kwani amecheza mechi nne tu chini ya Solskjaer tangu kocha huyo alipoanza kazi Man United Desemba, mwaka jana.


Wakala wa Sanchez, Fernando Felicevich, aliwahi kuteta na Juventus mapema majira ya kiangazi sanjari na Napoli, AC Milan.


Mchezaji huyo anataka kujiunga na klabu ambayo itampa nafasi ya kucheza akiwa na lengo la kuitwa timu ya Taifa kwa michuano ya Copa Amerika.


Sanchez amefunga mabao matatu katika mechi 32 alizocheza tangu alipotua Man United akitokea Arsenal.


Mshambuliaji wa zamani wa Man United, Robin Van Persie, alisema Sanchez anataka utulivu na kucheza katika klabu itakayompa furaha tofauti na Man United.


Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.