Na Shabani Rapwi


KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard amefunguka juu ya nyota wake Tammy Abraham kukosa penati katika mchezo wa UEFA Super Cup dhidi ya Liverpool.

Lampard amesema kukosa penati kwa mchezaji ni kawaida na aina maana kuwa kiwango chake ni kidogo, hivyo mashabiki awatakiwa kulaumu, badala yake ni kuunga mkono.

“Nilimwambia (Tammy) asiwe na wasiwasi…Nimekosa penati hapo awali, mtu yoyote anaweza kukosa, lakini ninachotaka kuona, kujiamini kwa mchezaji yeye kama mchanga na kupiga hatua”.

“Kukosa ni sehemu kuwa mchezaji katika kiwango cha juu, ambapo ndipo Tammy yupo sasa. Wakati huu unakuja na tunapaswa kumuunga mkono kwa sababu ndio mpira wa miguu”.

Chelsea ilipoteza mchezo huo wa UEFA Super Cup kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Liverpool baada ya dakika 120 kumalizika kwa kutoka sare ya 2-2, uliochezeshwa na mwana mama Stephanie Frappart.

Mlinda mlango wa Liverpool, Adrian ndio aliyekuwa shujaa katika mchezo huo baada ya kupangua penati ya mwisho iliyopogwa na Tammy Abraham na kuiwezesha Liverpool kutwaa Kombe la UEFA Super Cup kwa mara ya nne katika historia, (1977, 2001, 2005 na 2019).

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.