Uongozi wa Yanga SC wamjibu kocha wao Mwinyi Zahera baada ya kulalamikia michezo ya kirafiki ambayo Yanga SC iliicheza mkoa wa Kilimanjaro na Arusha haikuwa na msaada wowote kwenye kikosi chake.

Kupitia kwa Kaimu Katibu wa klabu hiyo, Dismas Ten aliweza kufunguka zaidi na kusema Zahera amezungumza vizuri lakini yawezekana alizungumza kwenye presha ya mechi lakini mpaka timu inasafiri kutoka Dar es salaam, kwenda Moshi na Arusha kwaajili ya mechi maanake ni kwamba benchi la ufundi lilikuwa na taarifa.

"Uongozi hauwezi kutengeneza mechi bila ya benchi la ufundi kuomba hizo mechi za kirafiki
Nakumbuka baada ya mchezo wa Township Rollers, hapa benchi la ufundi waliomba kuwepo kwa mechi za kirafiki, mchezo mmoja wa ndani na mchezo mmoja wa Kimataifa ili kuweka timu sawa kuondoa yale makosa ambayo yalijitokeza kabla ya mchezo wa marejeano kule Gaborone Botswana," amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Kwa hiyo niseme tu kwamba, hakuna ambacho kimefanyika nje na muongozo wa benchi la ufundi, kitu pekee ambacho naweza kusema ni kwamba, sisi tunaamini kwamba Michezo hii miwili imeleta picha nzuri zaidi kwenye benchi la ufundi hili kuweza kuiweka timu sawa na kwenda kujiandaa kwaajili ya mchezo wa marejeano na Township kule Botswana".

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.