WAPINZANI wa Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya UD Songo ya Msumbiji imewashtua Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya kushinda michezo yao miwili ya hivi karibuni ya Ligi Kuu nchini humo.

UD Songo inatarajia kuwasili nchini keshokutwa, kwa ajili ya kuikabili Simba katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumapili hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Beira, Msumbiji Agosti 10, mwaka huu, timu hizo zilitoka suluhu.

Matokeo hayo yameufanya mchezo wa marudiano kuwa wa wazi kwa timu zote.

Baada ya mchezo dhidi ya Simba,UD Songo imeshuka dimbani mara mbili katika michezo ya Ligi Kuu , ikianza kuichapa Chibuto mabao 2-0, mchezo uliochezwa Agosti 14 kabla ya kuwashushia kichapo cha mabao 2-0 mabingwa wa zamani wa nchini hiyo, timu ya Textile de Pungue, mchezo uliochezwa Agosti 18.

Leo itakuwa ugenini kukipiga na Clube Ferroviário de Nampula, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Campo da Bela Vista, mjini Nacala.

                                    

Wakati UD Songo wakishuka dimbani mara tatu mitatu kabla ya kukutana na Simba, Wekundu hao wamecheza mchezo mmoja wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Agosti 17, mwaka huu na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.

 

Hata hivyo, uongozi wa Klabu ya Simba umeshtukia hilo na haraka haraka   umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kushangalia mwanzo mwisho ili timu hiyo ipate matokeo chanya.

 

Katika mchezo huo ambao utaanza saa 10 jioni, viingilio vya vitakuwa mzunguko Sh. 5000, VIP B na C Sh 15,000, VIP A Sh 30,000, Platinum Sh 100,000 na Platinum Plus Sh 150,000.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara amesema tiketi kuelekea mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Alisema  pamoja na ubora wa kikosi chao msimu huu, lakini wanaiheshimu UD Songo kwakua ni moja ya timu ngumu hivyo wanahitaji nguvu ya ziada kutoka kwa mashabiki wao ili kuwaongezea morali ya kupambana wachezaji wao.

 

“Kwetu sisi Simba mashabiki sio mchezaji wa 12, bali shabiki anacheza kila namba uwanjani na wametufanya tumefika hadi robo fainali msimu uliopita, hakuna shaka kwamba tuna kikosi kizuri,lakini tunategemea zaidi nguvu ya mashabiki ili kufanya vizuri.

 

“Mafanikio yetu ya msimu uliopita yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na hamasa ya mashabiki wetu, ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye mechi zetu zote, lazima tukumbuke kuwa hii ni Ligi ya Mabingwa, hivyo si rahisi sana kupata ushindi hata kama upo nyumbani, lakini kwa nguvu za mashabiki, wachezaji na mapenzi ya Muumba basi tutaifunga UD Songo,” alisema.

 

Manara alisema pamoja na kuwataka mashabiki kuujaza uwanja, aliwataka pia kushangalia mwanzo mwisho ili kuwavuruga kisaikolojia wapinzani wasiweze kupanga mipango yao vema.

 

Simba itaingia uwanjani ikijivunia rekodi zake nzuri katika Uwanja wa Taifa kwani katika misimu miwili iliyopita ya mashindano ya kimataifa, haijapoteza mchezo.

 

Timu hiyo ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo msimu uliopita, baada ya kuvuna pointi tisa kwenye hatua ya makundi,baada ya kukushinda michezo mitatu nyumbani.

Katika michezo yake 12 ya kuanzia hatua ya awali hadi robo fainali msimu uliopita, Simba ilishinda michezo mitano nyumbani, sare mmoja, kupoteza mitano ugenini na kushinda mchezo mmoja ugenini .

Hata hivyo, UD Songo haina rekodi nzuri inapocheza ugenini kwani katika michezi sita waliyocheza msimu uliopita hawajafanikiwa kuondoka na ushindi, wakichapwa michezo minne na kutoka sare miwili.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.