KITENDO cha Paul Pogba kukosa penalti kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumatatu iliyopita, kimezua mtafuruku kiasi cha kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kufi kia kutoa uamuzi wa majukumu hayo kwa Marcus Rashford.
Solskjaer alikasirishwa na kitendo cha Pogba kukosa penalti hiyo, ambayo iliwakosesha ushindi katika kipindi ambacho matokeo yalikuwa 1-1.
Manchester United ndio ilianza kufunga kwa bao lililopachikwa na Anthony Martial katika dakika ya 27 wakati Ruben Neves aliisawazishia Wolves mnamo dakika ya 55. Matokeo hayo yaliifanya Manchester United kufi kisha pointi nne baada ya mechi mbili za ligi.
Pogba aling’ang’ania kupiga penalti hiyo licha ya kweli kuwa Rashford alikuwa na rekodi nzuri kwani ndio alipiga kwenye mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Chelsea na kufunga.
Hata hivyo, kwenye mechi na Wolves, Rashford alimwachia Pogba baada ya kutokea ubishi kati yao, ambapo alipokosa aliwaudhi wenzake na hata kocha Solskjaer, Taarifa zinasema kufuatia hali hiyo, Solskjaer aliwafokea wachezaji na kuwaeleza wazi kuwa Rashford ndio atakuwa mpigaji penalti namba moja wa timu hiyo.
Solskjaer alikwenda mbali zaidi kwa kuwalaumu Pogba na Rashford kwa kushindwa kutumia busara kupeana majukumu ya kupiga penalti. Pogba ndio alisababisha penalti hiyo kwenye mechi na Wolves baada ya kuchezwa rafu na beki wa kati wa Wolves, Conor Coady .
Kiungo huyo mfaransa akang’ang’ania kupiga penalti hiyo iliyookolewa na kipa wa Wolves, Rui Patricio.
Post a Comment