Kocha Zinedine Zidane amempa dakika nyingi za kucheza kwenye mechi za kujiandaa na msimu, lakini ni wazi kwamba bado anahitaji kuelewa namna ya kucheza na wenzake kikosini na cha kuvutia ni kwamba wachezaji waliong’aa katika mechi za kujiandaa na msimu ni Isco na Karim Benzema.

MADRID, HISPANIA . DIRISHA hili la uhamisho kwa Real Madrid hakika litatafsiriwa kwa usajili wa Eden Hazard, lakini bado kiungo huyo wa zamani wa Chelsea hajafanikiwa kuwashawishi wale wa mji mkuu wa Hispania.
Baada ya kutembea na sifa ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya England kwa muda mrefu, Hazard aliwasili kwa nderemo Madrid, hata hivyo ‘pre-season’ yake haijawavutia mashabiki wa klabu hiyo.

Kinachowapa hofu watu wa klabu hiyo si ishu yake ya kuwa fiti ama kuwa bonge nyanya baada ya kuongezeka kilo saba, kinachowatisha ni maswali kuhusu atakavyoweza kuizoea haraka timu mpya na mazingira mapya.
Kocha Zinedine Zidane amempa dakika nyingi za kucheza kwenye mechi za kujiandaa na msimu, lakini ni wazi kwamba bado anahitaji kuelewa namna ya kucheza na wenzake kikosini na cha kuvutia ni kwamba wachezaji waliong’aa katika mechi za kujiandaa na msimu ni Isco na Karim Benzema.
Yale makali yake hayajaonekana na awapo uwanjani, Zidane humhamishia Vinicius, jambo ambalo linalonekana kumfanya kinda huyo kupoteza makali yake akicheza upande huo.
Kutokana na Marco Asensio kutarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa tariban msimu mzima 2019/20, Zidane hana namna ili kutafuta utatuzi haraka iwezekanavyo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.