Mushami aliwaita wachezaji 10 wanaocheza soka nje ya Rwanda na 15, wanaocheza ligi mbalimbali nchini humo.
STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere na winga wa Yanga, Patrick Sibomana ni miongoni mwa nyota walioitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ kinachojiandaa kucheza mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Shelisheli.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Vincent Mushami ametangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaoingia kambini kujiandaa na mechi hiyo.
Mushami aliwaita wachezaji 10 wanaocheza soka nje ya Rwanda na 15, wanaocheza ligi mbalimbali nchini humo.
Kagere na Sibomana ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kuunda timu hiyo pamoja na Rwatubyaye Abdul (Colorado Rapids, Marekani), Nirisarike Salomon (FC Tubize, Ubelgiji), Bayisenge Emery (Saif Sporting Club, Bangladeshi), Muhire Kevin (Misr El Makkasa, Misri), Mukunzi Yannick (Sandvikens IF, Swideni), Bizimana Djihad (Waasland Beveren, Ubelgiji), Tuyisenge Jacques (Petro Atletico Angola), Hakizimana Muhadjiri (Emirates Club, UAE).
Tayari baadhi ya wachezaji wameingia kambini tangu Jumanne ya wiki hii, huku Kagere, Sibomana na wengine wakitarajiwa kujiunga na timu hiyo hivi karibuni ili kujifua kuikabili Shelisheli mechi itakayochezwa Septemba 5, mwaka huu Shelisheli ambapo marudiano itakuwa Septemba 10, Kigali, Rwanda.
Post a Comment