Na George Mganga
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema nafasi ya usemaji ndani ya klabu hiyo ipo chini yake mpaka sasa.
Manara ameamua kuliweka wazi hilo kutokana na uwepo wa taarifa katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari kuwa ataondoka kwenye nafasi hiyo.
Takribani wiki moja sasa imekuwa ikielezwa kuwa Mwandishi Gift Macha ambaye amekuwa akifanya kazi Azam Media anatajwa kuchukua nafasi ya Manara.
"Naomba ifahamike kuwa nafasi hii ipo chini yangu mpaka sasa.
"Siwezi kukaa Simba milele kwa kuwa hii ni klabu kubwa na yoyote anayefanya kazi hapa lazima ataondoka.
"Hii ni taasisi, ni kubwa kuliko mtu, si mimiwala si Crescentius Magori, wote tutaondoka".
Post a Comment