Guardiola alisema: "Namfahamu Sanchez. Tumefanya kazi pamoja Barcelona. Namkumbali sana kama mchezaji, lakini pia kama mwanadamu.

MANCHESTER, ENGLAND.KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amemtetea staa Alexis Sanchez akisema kwamba kuboronga kwa mchezaji huyo huko Manchester United halikuwa kosa lake.
Sanchez ameondokana na balaa la Man United baada ya kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa msimu wote wa kujiunga na Inter Milan katika dirisha hili la majira ya kiangazi.
Wakati fowadi huyo wa kimataifa wa Chile akilalamikiwa kila kona kwa kukosolewa kwamba kiwango chake kibovu kufuatia kucheza hovyo tangu alipotua Old Trafford akitokea Arsenal Januari, 2018, Guardiola ameibuka na kusema wanaopaswa kulaumiwa ni Man United.
Guardiola alisema: "Namfahamu Sanchez. Tumefanya kazi pamoja Barcelona. Namkumbali sana kama mchezaji, lakini pia kama mwanadamu.
"Ni mtu safi, mtaratibu na mpambanaji. Na sasa ameamua kwenda Italia kujiunga na moja ya timu kubwa Ulaya kwa sasa, Inter Milan, akicheza chini ya kocha mkubwa Antonio Conte.
"Nina uhakika mkubwa anakwenda kufanya vizuri kwa sababu namna ambavyo Inter wanacheza, unaonekana na mchezo wake. Kucheza karibu na Romelu Lukaku kwenye fowadi, naamini atakwenda kuwa na wakati mzuri huko Milan."
Guardiola alisema Sanchez hakupaswa hata chembe kubebeshwa lawama, kwa sababu soka ni mchezo wa timu na si mtu mmoja mmoja.
"Klabu ya soka haimtegemei mchezaji mmoja. Mnahukumu kwamba kufeli kwa timu basi ni Alexis, wakati kuna sababu nyinyine nyingi. Si vizuri kumnyoshea kidole mchezaji mmoja timu isipocheza vizuri. Hachezaji peke yake, sio tenisi wala gofu."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.