MADRID, Hispania

NYOTA wa zamani wa Chelsea, Eden Hazard, anaamini Christian Pulisic anaweza akawa moja wa wachezaji wazuri baada ya kukamilisha uhamisho wake akitoka Borussia Dortmund.

Dili la kumleta Pulisic jijini London lilikamilika Januari kabla ya Chelsea kukabiliwa na rungu na kutosajili lakini mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Marekani aliitumikia Dortmund kwa nusu msimu uliobakia kwa mkopo.

Pulisic alijiunga na wachezaji wenzake wapya katika maandalizi ya msimu mpya ziarani Japan ambapo alipangwa kwa mara ya kwanza na kocha Frank Lampard katika mechi dhidi ya Kawasaki Frontale na Barcelona.

Huku Hazard akishaaga baada ya kutumikia Chelsea kwa miaka saba, Mbelgiji huyo alimiminia sifa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 na anaamini atang’ara.

Akizungumza na The Associated Press , Hazard alisema: “Anaweza kuwa nyota. Sasa yupo katika moja ya klabu bora duniani. Ni mchezaji aliyekamilika. Anaweza kucheza mpira.”

Kinda huyo Mmarekani atakua na hamu kuvaa viatu vya Hazard lakini Pulisic anataka kijitengenezea jina kuliko kulinganishwa na mtangulizi wake.

Kocha mkuu, Lampard, ameanza kutengeneza kikosi chake kuelekea msimu mpya na mashabiki wanatarajia Pulisic kuwa na mchango mkubwa ndani ya Chelsea.

Uwezo wake na kupiga chenga unatajwa ni vitu ambavyo vitawasumbua mabeki wa timu mpinzani na kuwanyanyua mashabiki kwenye viti.

Chelsea walimnasa Pulisic kwa kitita cha pauni 58 na mchezaji huyo anayonafasi kubwa kukuwa kisoka chini ya jopo la makocha wanaosifika kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi.

Mason Mount na Fikayo Tomori waling’ara chini ya Lampard wakiwa Derby County huku msaidizi wake, Jody Morris, alipata mafanikio makubwa akiwa na kikosi cha vijana cha Chelsea.

Chelsea wanaendelea na maandalizi ya msimu mpya na leo wapo nyumbani kwa Reading inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kabla ya mchezo wao wa kwanza msimu 2019/20 dhidi ya Manchester United Jumapili ya Agosti 11. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.