KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwasasa anauwazia mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting na kubainisha kuwa kikubwa wanachokitaka ni kupata matokeo ili kuendelea kujiimarisha dhidi ya Zesco.
Yanga imewasili jijini Dar es Salaam alfajiri ya kuamkia leo ikitokea Botswana kucheza mchezo dhidi ya Township Rolles na kufanikiwa kupata matokeo yaliyowavusha hatua inayofuata kwa ushindi wa bao 1-0.
Akizungumza mara ya kuwasili nchini Zahera alisema wanasiku moja ya kukiandaa kikosi kwaajili ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Jumatano katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
"Tumewasili alfajiri wachezaji wanatakiwa kupata mapumziko ya siku moja kwaajili ya kupumzisha mwili kesho pekee ndio watafanya mazoezi ambayo hayatakuwa ya nguvu sana ili waweze kucheza mchezo huo," alisema na kuongeza kuwa.
"Hatuwezi tukaweka akili zetu kwenye mchezo wa Zesco wakati tuna majukumu ya ligi mbele yetu tunawaheshimu wapinzani wetu kwenye Ligi hata mashindano ya Ligi ya mabingwa lakini kikubwa ni hatua moja kufuata nyingine sasa tunaangalia Ruvu Shooting zaidi," alisema.
Post a Comment