Hatimaye ndoto  @smsuva27 zimeanza kutimia za kukipiga nje ya Afrika.

Wnga wa zamani wa Yanga, Simon Msuva anakaribia kutimiza ndoto zake  za kucheza soka la kulipwa Ulaya, mpaka sasa imefahamika kuwa mipango yake imeanza kutimia baada ya dili lake na klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu Ureno, kukamilika.

Meneja wa Msuva, Dkt. Jonas Tiboroha, amenukuliwa akisema,ni kweli Msuva anatarajia kujiunga na timu hiyo Januari mwakani na kwamba makubaliano yao itamtoa kwa mkopo wa miezi sita kwenda Panathiakos ya Ugiriki,
.
.........."Mwezi Janauri mwakani,Msuva atakuwa  katika timu ya Panathiakos ya nchini Ugiriki,atacheza kwa mkopo wa miezi sita baada ya kusajiliwa na Benfica"

alisema meneja wake Dkt Tiboroha.

Simon Msuva kwa sasa anakipiga katika timu ya Difaa El-Jadida ya Ligi Kuu ya Morocco, iliyomsajili mwaka 2017 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga sc ya Tanzania.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.