Katika kukiongezea makali kikosi cha Simba kunako safu ya ushambuliaji, inaelezwa mabosi wa klabu hiyo wako kwenye mchakato wa kuongeza winga mmoja wa nguvu.

Mkongomani Rossein Tuisila Kisinda anayekipiga AS Vita ya Congo, anatajwa kuwa katika rada za mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara na kuna uwezekano akashushwa hapa nchini dirisha dogo.

Kisinda ni straika anayecheza kama winga na inaelezwa amekuwa akiwaniwa na baadhi ya timu zingine nje ya Congo ili kupata huduma yake.

Mabosi wa Simba wanavutia zaidi nguvu kwa winga huyo huku mchezaji mwingine ambaye bado bado jina lake halijafahamika ni kutoka KCCA ya Uganda.

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Disemba 16 mwaka huu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.