Wakati Simba na Lipuli zikiteremka uwanjani leo kuwania pointi tatu, vita kubwa ipo kwa washambuliaji Meddie Kagere na Paul Nonga.
Simba na Lipuli ya Iringa zitavaana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kivutio katika mchezo wa leo ni vuta ya ufungaji mabao baina ya Kagere (Simba) na Nonga ambao wamekuwa na viwango bora msimu huu.
Kagere anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao manane na Nonga saba, hivyo kila mmoja atakuwa na shauku ya kufunga ili kuboresha akaunti yake.
Pia mchezo huo utawakutanisha washambuliaji wawili Miraji Athumani wa Simba na Daruwesh Saliboko ambao kila mmoja amefunga mabao sita. Miraji amekuwa na kiwango bora na ndiye aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya ligi kusimama kupisha mechi za timu ya taifa.
Saliboko ndiye mkombozi wa Lipuli kwani amekuwa akifunga mfululizo na ameingia katika orodha ya wachezaji watatu waliofunga ‘hat trick’ msimu huu akiungana na Ditram Nchimbi na Obrey Chirwa. Timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa kutokana ubora wa vikosi vyao huku rekodi baina yao ikizidi kuongeza ushindani wa mchezo wa leo

Post a Comment